Ukweli kuhus Nguva....... (Je ndie yule Samaki Mtu???)

Published on by Boniventure Mchomvu

Ukweli kuhusu nguva huu hapa….!!!! Nguva au “ng’ombe wa baharini” ni viumbe wa baharini ambao hukua hadi kufikia mita 3 kwa urefu na uzito unaoweza kufikia kilo 400 hadi 500. Jina la ngo’mbe wa baharini linatokana na ukweli kwamba nguva hula majani ya baharini ambayo hutengeneza nyanda za malisho kwenye maji ya pwani zilizotulia. Kadri Nguva wafanyavyo malisho, hung’oa mmea wote na kuacha alama ya sehemu walizokula, hivyo kwa watafiti inakuwa rahis kuweza kufuatilia malisho na makazi ya nguva kwa kufuata walizokula. Nguva wana rangi ya kijivu na udongo, rangi ya kijivu imekolea zaidi sehemu ya juu kuliko ya chini. Nguva wanalekea kufanan na na pomboo (Dolphin) na wana pua kubwa iliyo fupi. Nguva yupo katika kundi la mamalia na sio samaki, pia muonekano wa nguva si kama inavyoaminika na waliowengi kuwa ni nusu samaki, nusu binadamu (mwanamke). Nguva huishi kwenye maeneo ya kina kifupi katika maji ya tropiki (katika nchi za joto) katika maeneo yote ya Bahari ya Hindi na Pasifiki. Katika ukanda wa Afrika ya mashariki, nguva wana hatari kubwa ya kutoweka kutokana na kukamatwa kwenye nyavu za uvuvi hususani nyavu aina ya jarife, kuwindwa na pia uharibifu wa maeneo yao ya malisho yao. Ikiwa nguva atakamatwa kwenye nyavu iliyotegwa chini ya maji, hufa mara moja kwa kukosa nafasi ya kuja juu kuvuta hewa, hii ni kwa sababu nguva sio samaki na hawezi kupumua ndani ya maji, anahitaji kutoa pua yake juu ya maji ili kuvuta hewa na kisha kuzama tena majini. Kama ilivyo kwa binadamu, na tembo, nguva wanaweza kuishi maisha marefu hadi kufikia miaka 70.Nguva huzaa mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka kati ya 10 hadi 17. Hubeba mimba kati ya miezi 13 hadi 15 na huzaa mtoto mmoja tu. Ndama aliyezaliwa anaweza kufikia uzito wa kilo 30 na hunyonya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu hadi mitatu. Endapo nguva jike atazaa mtoto dume atahitaji kujitenga na kundi la nguva wengine kwa kuhofia mtoto wake kuuwawa na dume kubwa katika kundi, hivyo atakaa mbali na kundi hadi pale mtoto wake atakpokuwa na uwezo wa kujihami n dume kubwa katika kundi, hii ni kama ilivyo kwa kiboko. Nguva ataendelea kuzaa kila baada ya miaka 3 hadi 7. na hunyonya kwa muda wa karibu miaka miwili. Nguva huogelea kwa kutumia mkia wake bapa kama wa nyangumi akisaidiwa na mapezi ya mbele kwa kujihimili na kugeuka. Mwendo wao ni wa taratibu sana. Wachunguzi na mabaharia wa mwanzo waliamini kuwa nguva walikuwa nusu watu kwa sababu ya miili yao iliyoumbwa kwa umaridadi pamoja na matiti makubwa chini ya mapezi yao. Wana kichwa cha mviringo na macho madogo na pua zao ziko juu ya mdomo, na kama wanyama wengine, nguva ni lazima aibuke juu ya maji ili kuvuta pumzi. Tofauti na wanyama wengine wa majini kama vile nyangumi au pomboo, nguva hawezi kuzuia pumzi kwa muda mrefu haswa anapokuwa anaogelea kwa kasi. Nguva wana uwezo mdogo wa kuona lakini wana uwezo mkubwa wa kusikia. Hutafuta na kula majani ya baharini kwa kutumia sharubu ngumu zenye hisia kwenye mwili wake ambazo zinafunika sehemu ya juu ya mdomo wake. Meno yao kama vipembe yanaweza kuonekana haswa kwa nguva dume na baadhi ya majike yenye umri mkubwa. Wakati wa kipindi cha kuzaliana nguva dume hutumia vipembe vyao kupigana na dume mwenzake. Chakula kikuu cha nguva ni majani ya bahari. Kwa hiyo hutumia muda wao mwingi wa malisho kwenye maji mafupi na kwenye matumbawe na sehemu ambazo maji ya mto huingia baharini. Mojawapo ya maeneo muhimu ya nguva hapa Tanzania ni delta ya Mto Rufiji. Hali hii hupelekea nguva kukutana sana na shughuli za uvuvi, maana sehemu ya malisho yake ndio sehemu wavuvi wengi wanatega mitego yao ya uvuvi hususani jarife. Nguva wanahifadhiwa rasmi chini ya sheria ya taifa (Sheria ya Uvuvi) na wameorodheshwa na Shirikisho la Uhifadhi Duniani (IUCN) kama wanyama walio katika tishio la kutoweka. Hata hivyo kutokana na miaka mingi ya kuwawinda kupita kiasi idadi ya nguva nchini imepungua kupita kiasi. Jitahada zinafanyika kuchunguza hali ya nguva nchini kwa kwenda kufany tafiti katika maeneo yaliyoripotiwa kuonekana ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano na wenyeji ili kuelewa vizuri ukubwa wa idadi yao kwa sasa, upatikanaji wao na hatari zinazowakabili. Wavuvi waliomnasa nguva katika nyavu za jarife – Mafia Kwa kuangali na kuona umuhimu wa kuendelea kuwa na nguva Tanzania Sea Sense iliamua kuanzisha mtandano wa ukusanyaji wa taarifa za nguva, amabo unajumuisha wavuvi na wanavijiji. Lengo la mtandao huu ni kuweza kupata hali halisi ya upatikanaji na uwepo na idadi ya nguva Tanzania ikiwa ni pamoja na kujua madhara yanayowakabili. Tangu kuanzishwa kwa mtandao huu mnamo mwaka 2014, Nguva 55 wameripotiwa, 40 kati yao wakiwa wazima/hai (wakiwemo majike wawili na ndama wao), wakati 14 wakiwa wamenaswa na nyavu za jarife na hatimae kufa ( akiwemo jike mmoja na ndama wake), wakati mmoja alionekana akiwa amekufa na kutupwa ufukweni. Kwa taarifa hizi inadhihirisha kuwa bado kuna idadi ndogo ya nguva inayopatikana Tanzania, Rufiji na Mafia. Wavuvi wakiwa nanguva waliyemvua huko Mafia Ili kuhakikisha kuwa wavuvi na jamii ya wavuvi wantambua umuhimu wa uhifadhi wa nguva, Sea sense imetoa elimu hiyo kwa wanajamii ikiwemo kuweza kutoa taarifa pindi wamuonapo au kumakamata nguva. Kampeni hii ya utoaji elimu imeelekea kufanikiwa kwa kiasi, kwani baadhi ya wavuvi wamekuwa wakitoa taarifa za uonekanaji na upatikanaji wa nguva na hapo kufatilia kwa ukaribu na kuweza kujiridhisha na taarifa hizo kwa kushirikiana na wavuvi waliotoa taarifa. Kwa sasa taarifa nyingi za uonekanaji wa nguva zinapatika kutoka mafia na delat yam to Rufiji. Ktaika ya miaka ya 70 na 80 Nguva walikuwa wanapatikana na kuvuliwa katika ukanda wote wa pwani Tanzania. Lakini kwa kuwa kasi ya uvunaji na uharibifu wa mazingira imekuwa kubwa sana, idadi ya nguva imekuwa ndogo sana na kwa sasa wanaonekana katika sehemu mbili tu yaani Mafia na Rufiji. Gwaride la nguva kwa wananchi ili kumjua nguva halisi na sio fikra potofu walizokuwa nazo - Mafia Hata hivyo kuna baadhi ya wavuvi wamekuwa wakiogopa kutoa taarifa za nguva pindi wanapomuona wakidhani ya kuwa eneo hilo litazuiliwa kwa shughuli za uvuvi ili kuhifadhi nguva. Ukanda wa pwani ya Tanzania una wastani wa zaidi ya watu million kumi ambao hutegemea uvunaji wa rasilimali za pwani na baharini katika kuendeshsa maisha yao. Nyma ya nguva inaaminiwa kwa kuwa nap rotini nyingi na bei yake ni kati ya 5,000 hadi 8,000 kwa kilo. Hivyo kutokana na mahitaji makubwa ya nyama ya nguva imekuwa vigumu sana kwa wavuvi kumuachia nguva pindi anaponasa kwenye nyavu za uvuvi. Kwa namna hii elimu zaidi inahitaji kwa jamii ya ukanda wa pwani ili kuweza kujua umuhimu wa kuhfadhi nguva kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho. Duniani nguva analindwa chini ya usimamizi na udhamini wa mashirika ya uhifadhi duniani ikiwemo IUCN, CMS and mengineyo. Tanzania ikiwa kama mwanachana na kusaini mikataba na mshirika hayo juu ya usimamizi na uhifadhi wa nguva na makazi yake, Tanzania ilikuwa miongozi mwa nchi za kwanza kusaini makubaliano hayo mnamo mwaka 2007, zaidi ya nchi 14 sasa hivi zimeingia katika makubaliano hayo. Ili kuhakikisha kuwa makubaliano yanatekelezeka, 2010 tanzania ilianzisha kamati ya kitaifa ya uhifadhi wa kasa na nguva Tanzania (TTDCC). Hii ikiwa ni kuhakikisha kuwa kuna kuwa na fursa kwa wadau kukaa pamoja na kutekeleza usimamizi na uhifadhi wa idadi ndogo ya nguva iliyopo hapa Tanzania. Nguva aliyenaswa na nyavu ya uvuvi na kisha kufa – Rufiji

Nguva aliyenaswa kwenye nyavu za jarife huko kisiwani mafia, nyavu hizi ni tishio kubwa kwa uhai na maisha ya nguva baharini
Nguva aliyenaswa kwenye nyavu za jarife huko kisiwani mafia, nyavu hizi ni tishio kubwa kwa uhai na maisha ya nguva baharini Nguva aliyenaswa kwenye nyavu za jarife huko kisiwani mafia, nyavu hizi ni tishio kubwa kwa uhai na maisha ya nguva baharini Nguva aliyenaswa kwenye nyavu za jarife huko kisiwani mafia, nyavu hizi ni tishio kubwa kwa uhai na maisha ya nguva baharini

Nguva aliyenaswa kwenye nyavu za jarife huko kisiwani mafia, nyavu hizi ni tishio kubwa kwa uhai na maisha ya nguva baharini

To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post