Mwongozo wa Taifa wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Tanzania.

Published on by Boniventure Mchomvu

Wataalamu na wadau wa uvuvi_Mkonge Hotel, Tanga

Wataalamu wa uvuvi Tanzania wakipitia na kuandaa mwongozo wa Taifa wa usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi Tanzania. Mwongozo huu unatokana na miongozo iliyokuwepo mwanzo ambapo awali kulikuwa na miongozo ya kanda mbalimbali za maji baridi na maji chumvi (baharini) na pia ule wa usimamizi wa kambi za uvuvi pamoja na mwongozo wa usimamizi shirikishi wa maeneo ya pamoja. 

Kwa mkutano huu wa siku tano uliofanyika Jiji Tanga katika hoteli ya Monge, timu hii ya wataalamu wauvuvi kutoka secta za Serikali kuu, Halmashauri za Wilaya, asasi za kijamii, taasisi za elimu na wanajamii, inatarajiwa kuja na mwongozo wa kitaifa ambao utaongoza shughuli zote za usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi. Mwongozo huu utatumika sambamba na utekelezaji wa sera ya uvuvi, sheria na kanuni zake katika usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi. 

Mwongozo huu unatoa fursa kwa wadau kusimamia, kutumia na kuendeleza rasilimali za uvuvi. Jamii ya wavuvi ikiwa kama mmiliki na mtumiaji wa rasilimali hizi ina pata wasaa wa kuziangalia kwa jicho la karibu kwa kuwa ndie aliyeko karibu zaidi na rasilimali hizi huku akiwa na uelewa mkubwa wa rasilimali hizi hivyo kuwa na uwezo na nafasi kubwa ya kuzisimamia kwa weledi. 

Hii ni katika harakati za serikali kutoa nafasi kwa wanajamii kushirki moja kwa moja katika kulinda na kuendeleza rasilimali zao kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Pia inatoa nafasi kwa jamii kutambua raslimali zao na pia kuweza kufanya tathmini ya rasilimali hizo na kufanya maamuzi sahihi kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo. 

Wataalamu wanaamini kuwa kwa mwongozo huu jamii itaweza kumiliki na kusimamia rasilmali zao kwa weledi na ufanisi mkubwa huku jamii ikiinua kipato chake na kuboresha maisha yao pia ikitekeleza farsafa ya uhakika wa chakula kwa kuwa na rasilimali endelevu. 

To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post